Translation Games: Kiswahili

20 8 1
                                    

Mkutano

FoolsErrand

Iliyotafsiriwa na Lujayna


Kimya kilichotarajiwa kilianguka kwenye mkutano wa Miungu lilipowasili Umbo la kumetameta.

"Labda yeyote angependa kusema maneno mafupi?" Umbo liliuliza kwa ubusara.

Miungu hawana mabuti na lau wangekuwa nayo, yangekuwa ishara ya kuwa wanaangalia upande wake.

"Tuanze," lilisema Umbo kwa kusinywa, likiwa linavunja hicho kimya cha kioja.

Umbo hilo la ajabu lilipanuka kwenye ulimwengu na kujikunja kama kamba nyembamba kwenye nyota inayojulikana kama jua. Lilisangaa kwa kusisimua na halafu, kwa vishindo, lilizima hilo jua.

Miungu walimaka, nafuu ikiwaenea.

Umbo hilo lilinong'ona kwa dhihaka, "Hatimaye kuna amani."

Tevun-Krus #97 - International VI: PeaceWhere stories live. Discover now