Sura ya Kumi na Nne

23 1 0
                                    

Byongo na Malkia walikuwa wanagenzi katika vyuo tofauti mjini Nairobi.
Byongo alikuwa akisomea uhadisi wa kopyuta huku Malkia akisomea utabibu katika chuo cha utabibu cha hospitali kuu ya Kenyatta.
Malkia alikuwa banati mpole,mwenye hatua za kuhesabika kila alipotembea.
Mtindo wake wa adabu na heshima,upole wake katika gumzo,ulimvutia kila aliyetangamana naye.
Kila alipowasalimu wakubwa wake, Malkia alikunja magoti yake na kuinamisha kichwa,ishara ya unyenyekevu.
Alizua umaarufu kila alikokwenda kwa hulka yake ya Kiganda.
Malkia alikuwa kifungua mimba wa Zuhuria na Mathangi.
Alikuwa ameenda mjini Nairobi kwa kuwa kule nchini mwao,hamukuwa na vyuo, kutokana na hali ya mshikemshike iliyoshamiri kwa kipindi kirefu.
Ni kinaya kilichoje kwa nchi yenye madini na hata visima vya mafuta kutokuwa na miundo misingi katika takriban nyanja zote?
Ni kielelezo cha tamaa ya vigogo watawala wanaopanua vinywa vyao kuyajaza matumbo yao bila kuwajali walala hoi.
Visima vya mafuta viligeuzwa visima vya laana,huku waliowengi wakishuhudia mifereji ya kusarisha mafuta ikitapakaa kila mahali,ila pasiwe na mfereji hata mmoja wa maji safi.
Vidimbwi vilivyoachwa wazi baada ya kuchimbwa madini viligeuka makaburi ya kuwameza wakaaji wangali uhai.
Mibabe wa kivita walifyonza hela za mafuta na kununua majumba ya kifahari katika nchi jirani.
Familia zao ziliishi kifalme,huku waliowengi wakiishi kwenye majumba yaliyojengwa kwa uchochole.
Kuta za uchochole,sakafu za umaskini na paa za fedhea.
Wana wa mibabe ya kivita, walisomea shule na vyuo katika nchi zingine,huku wana wa 'wenye nchi' wakibaki kutazama magari ya mibabe hao yakipitana vijiani.
Walivaa maganda au hata kuvalia uchi wao huku wakionekana kusalim amri kuwa hali zao zilikuwa majaliwa.
Waliyala mate yao ili kukinai kila siku.
Wavulana wa kuanzia umri wa miaka kumi,waliingiwa katika makundi ya kivita na kugeuzwa kuwa makombora ya kulindia rasilmali za mibabe hao,ili familia za mibabe zisikose chakula wala masomo.
Byongo na Malkia wote walituwa na mizizi kuto nchi Ile, hivyo kuwa rahisi kwao kufahamikiana.
Byongo hakumfahamu babake,ila mamake alikuwa akimliwaza kuwa ni daktari katika mji mmoja kule Kenya,ila mawasiliano yao yalikatika,asijue yu hai au kafa.
Byongo hakuwahi kuiona hata picha ya babake, hivyo kwake,mamake alikuwa ndiye baba na mama.
Licha ya mamake kumtimizia yote mahitaji,mwoyoni alikuwa na ombwe tupu,ambalo lingejazwa tu,kwa kumwona babake.
Mamake Byongo alitokea sehemu za Nyanza nchini Kenya na alikuwa akilifanyia kazi shirika moja lisilo la kiserekali kama mhasibu.
Usuhuba baina ya Byongo na Malkia,ulikuwa umekita mizizi wakawa wakishirikiana katika mambo mengi.
Wakati wa likizo, Byongo alikuwa akikaa kwa wazazi wa mamake.
Huku alipenda sana kufuga mifugo na kuwasaidia wazee wake shambani.
Kwa upande wake, Malkia alitumia likizo zake kwa shangaziye mjini Nairobi.
Masomo yao yaliendelea bila kasheshe yoyote na walitarajia kuhitimu kwa wakati uliopangwa.

*********************************
Lucia,mamake Byongo, alikuwa katika mwaka wake wa tatu katika chuo kikuu mjini Eldoret alipokutana na jamaa mmoja ambaye alijitambulisha kwake kama Fredie.
Fredie alimpata Lucia barabarani akitembea kuelekea chuoni kutoka mahali alikokuwa akiishi,nje ya chuo.
Kutokana na idadi kubwa ya wanafunzi chuoni,Lucia hakuweza kupata chumba ndani ya chuo, hivyo kulazimika kutafta malazi mbadala viungani mwa chuo chake.
Alibahatika kupata chumba cha bei nafuu, takriban mwendo wa matembezi ya dakika ishirini kutoka chuoni.
Ni katika safari moja wapo wa safari zake za kila asubuhi, alikokumbana na Fredie,aliyemsihi kusafiria gari lake,ili amfikishe chuoni,kwa kuwa pia yeye alikuwa akielekea kule kule.
Baada ya kumsihi kwa muda,Lucia alikubali kuingia kwenye gari na kupewa lifti.
"Hi waitwaje dadangu?Mimi ni Fredie, daktari wa kibinafsi huku mjini" Fredie alimpekuapekua Lucia,huku akimperemba kwa macho na kumwacha uchi.
"Am Lucia, mwanafunzi  mhasibu hapa chuoni" Lucia alimjibu Fredie huku akiinuka kidogo na kuivuta sketi yake kuyasitiri mapaja yake.
Macho ya Fredie yalifuata harakati zake zilizoambulia patupu,kwani sketi yenyewe ilikuwa fupi,hivi kwamba kujaribu kuiteremsha kulikuwa sawa na kujaribu kuivua.
"What a beautiful name!So what do you do to relax on weekends?" Fredie aliendeleza ujasusi wake.
"Sinaga shughuli mob,mara nyingi ni kupumzika tu kwangu,kutembelea marafiki humu humu chuoni,au kucheza TT " Lucia alijibu huku akionyesha kutulia.
"Can I have your number please!We can do coffee this weekend and get to know each other better.Am here to see a friend na kisha nirudi mwangu kazini"
Lucia alishuka kutoka kwa gari na kuelekea zake masomoni huku Fredie akijipa hamnazo, kuelekea jengoni lililokuwa na maofisi.
Huu ukawa mwanzo wa urafiki ambao ulikita mizizi kati ya Fredie na Lucia.
Urafiki ambao baadaye ulitumbuka nyongo na kumwachia Lucia na ujauzito.
Ujauzito uliomleta Byongo humu duniani.
Fredie na Lucia waliwahi kukutana mara si haba kule mjini.
Mikutano yote ilikuwa mikawani na Lucia alikuwa macho ili asianguke kwenye mitego ya vileo,na kuishia kujuta kama alivyokuwa ameskia katika masimulizi kule chuoni.
Kumbe Fredie kwa upande wake alikuwa kama panya,apulizaye kabla ya kutafuna viganja vya mtoto usiku wa manane.
Fredie alikuwa na mpango  'water proof' kumnasa Lucia.
Fredie aliandaa karamu ya kusherehekea siku ya kuzaliwa kwake na kuwaalika marafiki zake, akiwemo Lucia.
Ilikuwa karamu ya kukata na shoka iliyoandaliwa katika nyumba moja ya kifahari,ambayo licha ya Fredie kumjulisha Lucia kuwa ilikuwa nyumba yake, ilikuwa uongo mweupe pepepe!
Alikuwa ameikondisha kwa shughuli hii ya karamu tu!
Ni siku ya iliyokuwa ya kwanza kwa Lucia kuka maji.
Mwanzo, mwanzo,alihisi kichefuchefu kwa ukali wa mvinyo, lakini baada ya mafunda kadhaa,na kusinikizwa na wenzake,akazoea na kubugia mvinyo uliomwacha mlevi chakali, hajijui hajitambui.
Hivyo ndivyo alivyoamkia kitanda asichokifahamu,kando yake,Fredie akiwa uchi wa mnyama aking'orota kama nguruwe.
"Hoo my God,where am I?What happened?Fredie...Fredie.." alimgongagonga Fredie na kumwamsha.
Aliinua shuka na kupigwa butwaa kuwa alikuwa uchi wa tumbili.
"We made love honey,it was the best thing that happened.We were so passionate" Fredie alisema huku akimkumbatia.
"Bila Kinga?...what if .." Lucia alionyesha kumaka.
"Hakuna what if... everything will be fine" Fredie alimtuliza.
"I need to go!"
"You took advantage of me? Lucia aliamka na kujaribu kuzivaa nguo zake upesiupesi.
Akipepesuka na kuegemea ukutani.
Alitamani kwenda bafuni na kujisugua kwa sabuni ili kuondoa fedhea lakini miguu yake ikaganda kwa uzito.
"Just relax...take some fruits,halafu nitakudrop!"
Lucia aliketi kitandani,kichwa mikononi.
Alikuwa anaona kizunguzungu.
Kichwa kilisikika kama jabali zito alilolibeba kichwani.
Ni kana kwamba moyo wake ulikuwa ukidundia utosini.
"Naomba maji tafadhali"
Fredie alinyanyuka kwa mpepesuko na kumwandalia Lucia kikombe cha maji ya matunda.
Baada ya kuyanywa alirudi kitandani na kulala usingizi wa pono.

Gilasi yake ilikuwa ivunjwa,jambo lililomtia ghadhabu,haya na majuto kwa pamoja.
Ulikuwa mkusanyiko wa hisia akilini mwake.
Usingizi ulimbeba angalau kumpumbaza kwa muda.
Majuto ni mjukuu huja baada ya kitendo.
Hivyo ndivyo Lucia aliupoteza ubikira wake na juu yake kuambukizwa mimba asiyeipangia wala kutamani.
Kuchoma mwiba juu ya doda sugu,usiku huu ulikuwa wa mwisho kumuona na  kumsikia Fredie.
Fredie akitokomea kama kiza majio ya jua.
Simu yake ikawa mteja na malazi akahamisha.
Fredie alikuwa mwindaji anayemwandama swara,na kisha kuhamishia mtego wake kwingineko,mara tu baada ya kumnasa.

************************************
Ni tukio ambalo liliwapiga waliokuwepo kama radi ya masika.
Lucia na Mathangi walitamani ardhi kupasuka na kuwameza wazima wazima.
Yaliyokuwa machoni mwao yalikuwa haramu,haramu ya matunda ya tendo lao miaka mingi iliyotangulia.
Lucia alijawa na hamaki, zile zile za miaka ya chuoni,alipopachikwa mimba.
"You bastard,Fredie,singedhani tutakutana baada ya miaka hii yote,tena katika mazingara kama haya" Lucia atamka kwa hamaki na kumuezeka Mathangi kofi lililomwacha amizungukiwa na dunia na kuona vimulimuli.
"Nini kinaendelea jamani,what's happening?" Zuhuria alishangaa huku akimuinua Mathangi kutoka sakafuni alikokuwa amelazwa kwa kofi la Lucia.
"Mum, tafadhali,tueleze kinachoendelea,why have you hit baba Malkia?" Byongo alimsihi mamake huku akimkamata na kumutuliza.
"Yarrabbii! Leo laana imetupata"
"Kaka kamchumbia dadake!"
"Turehemu Maulana. Lucia atamka huku akijimwaya sakafuni kwa majuto.
"I don't understand,can someone explain to us please!" Malkia aliuliza huku akishika kichwa chake kwa mikono yote miwili.

Baada ya kutulia Mathangi, samahani,Fredie, samahani tena, Mathangi Fredie, alielezea jinsi alivyomlaghai Lucia na kumwachia ujauzito.
Byongo alikuwa kijana wa Fredie Mathangi.
Byongo alikuwa ndugu yake mchumbake, Malkia.
Vijasho viliwatoka Byongo na Malkia wakaona ni kana kwamba walishiriki katika sinema au mchezo wa kuigiza.
Mathangi alipigwa na butwaa,haja zote mbili;kubwa na dogo zikamtoka kwa pamoja.
Ujogoo wake ulikuwa umemzalia matunda ya mti wa fedhea na laana.
Vitendo vyake vya zamani vikawa vimemfikia baada ya kumwandama kwa miaka mingi.
Ilikuwa ni siku iliyotarajiwa kuwa ya furaha kwani Byongo, alikuwa amemkaribisha mchumbaye kwa nyanyake,Nyanza,ili,kuwatambulisha wazazi wa pande zote mbili.
Wazazi wao wakatukia kuwa mama wawili,baba mmoja.
Wavyele walipendekeza pafanyike tambiko, ili kuiepushia familia hasira za miungu,hasa ikiwa,wachumba haya, walikuwa wameila asali ingalipo mzingani.
Byongo na Malkia walisisitiza hawakuwa wamevuka mpaka.
Licha ya wazazi wao kuwaamini,tambiko lilifanywa na wazee.
Byongo alikuwa amepata nafasi ya kumjua babake, nafasi alioitamani tangu utotoni.
Alilokuwa halijui ni kuwa angemjua babake kapitia vurumai la kihistoria.
Baba ni yupi?
Aliyezalisha au aliyelea?
Je kuna uwezekano wa  kumwita mzazi aliyelea pekee yake,mamababa au babamama?
Je ni haki kumuita mwana haramu, kutokana na tendo la haramu?
Mwana ni mwana,kitendo ndicho cha haramu.

SUZANNAWhere stories live. Discover now