Sura ya Kumi

20 0 0
                                    

"Rais wa Marekani,Barrack Obama,First lady Mitchell,Katibu mkuu wa UN,Katibu mkuu wa UNHCR,viongozi wote wa kimataifa walio hapa,wakereketwa wa haki za kibinadamu,mabibi na mabwana"
"Baada ya miezi sita ya kutadhimini na kuwapigia upato washirikishi mbali mbali,leo tumekusanyika hapa ili kumtunuku mshindi wa taji la Umoja wa Mataifa kuhusu ukereketwa wa haki za kibinadamu"
"Kabla ya kumtaja mshindi tutazame habari kuhusu washindani wetu watano wanaomenyania nafasi ya kwanza."
"Ikumbikwe tulipokea udhamini wa wakereketwa zaidi ya mia tano kutoka pembe zote za dunia, ila tulichagua mia,ambao walipigiwa kura,kisha tukabaki na kumi bora zaidi"
"Naomba tuangazie kwenye Runinga tutazame hadithi za watano wa kwanza" alisema kiongozi wa hafla Bi.Oprah.
Hadithi kuhusu Hafsa ilikuwa ya tano kuangaziwa,na katika orodha.
"Bi.Hafsa ni mfano wa mti uliomea kando ya barabara,panapopitia watu.Mti unaokomaa  kutokana na mche hadi uzima licha ya kukanyagwa na wapita njia."
"Hafsa alizaliwa na kuwapoteza wazazi wake akiwa mdogo.Alichukuliwa na Mjombake aliyemwoza kwa jizee la umri wa babuke.Alikeketwa na kisha kuozwa kulingana na tamaduni za jamii yake."
Machozi yaliwalengalenga watazamaji machoni kwa picha na maneno mazito yenye kukamua hisia zao.
"Hafsa aliweza kuokolewa na kurudishwa shuleni ambako alitia fora"
"Alisomea Uanasheria kule Saudia na kuhitimu"
"Hafsa alianza kujishughulisha na ukereketwa wa haki za mtoto msichana akiwa bado chuoni"
"Baada ya kuhitimu alirudi kwao Kenya,ambako ijiunga na utangazaji wa habari"
Kwa Sasa Hafsa alishikilia roho yake mikononi.
Suzzanna aliwekelea mkono wake juu ya mkono wa Hafsa ili kumpa moyo.
"Amekuwa akiandaa kipindi cha mahojiano kufahamisha na kuangazia haki za binadamu"
"Kupitia kipindi chake amewahamasisha watazamaji kuhusu haki zao za kinadamu,kukashifu ukiukaji wa haki na pia kuisindikiza serikali kuchukua hatua kwa wanaokiuka haki hizo"
"Hafsa pia ameweza kwa kushirikiana na wenzake kupindua tamaduni potovu, zinazowachukulia wasichana na wanawake kama vifaa vya kimapenzi,nchini mwake na kote duniani."
"Hafsa ni shujaa mkereketwa"
Baada ya hadith hii,watu wote walisimama na kupiga makofi kwa msisimuko.Ikawa ni kana kwamba mshindi ametangazwa.
Machozi ya furaha yalimtoka Hafsa machoni na likawa jukumu la Suzzanna kuyapangusha yasimfike mashavuni.
Pamoja na Suzzanna, wengine walihudhuria tuzo hili ni:Bundi,Maria,Jason na Chris.
"Haya haya, naomba tuketi kwani ndio mwanzo chungu kimetokota"
"Bado hatujamjua mshindi hata ingawa washiriki wote mia tano, waliopendekezwa tayari ni washindi"
"Tutakaye mtaja dakika chache zijacho ni wa kwanza kati ya washindi mamia ya maelfu,kote duniani,wanaojizatiti kila siku kutetea haki za binadamu." Bi.Oprah alisema huku alimkaribisha Bi.Mitchel Obama kufika mbele kumtangaza mshindi.
Rais Obama kama kaida yake, alimshika Mitchell mkono na kumsindikiza hadi jukwaani na kisha kusimama kando yake.
Makofi na tabasamu viliandamana nao kutoka walikoketi hadi jukwaani.
Baada ya hotuba yake Mitchell, ya kukata na shoka, wakati wa kumtaja mshindi ukafika.
"Ladies and gentle men,the winner of this year's,United Nations Human Rights Activist is...."alitamka Mitchell na kuwaacha wasikizaji wakininginia kwa hamu ya kujua.
"Ili kutambua juhudi na imani aliyonayo Rais,mume wangu Barrack,namuomba aje aifungue bahasha hii" Mitchell alisema huku akimgeukia mumewe na kumshika mkono ili kumkaribisha.
"And the winner is..." Obama alionyesha kikaratasi kilichoandikiwa kwa herufi za mlazo,"HAFSA KUTOKA KENYA"
Hafsa alipiga magoti kana kwamba anaswali kwa kutoyaamini macho wala maskio yake.
Suzzanna alimwinua na kumpandisha jukwaani.
Alipigwa pambaja zisizohesabika na kupongezwa na wote.
Alitunukiwa taji na akaombwa kusema.
"Taji hili ni la watoto wote,wa kike na wa kiume"
"Ya kwamba haijalishi mazingara uliyozaliwa na kulelewa.Haijalishi matatizo unayoyapitia"
Alipanguza machozi huku akimkabidhi Suzzanna taji kushikia.
"Ukitia bidii,kuwa na matumaini na kumuomba Allah,iko siku njema itakayofika" Hafsa alimalizia huku washiriki wakisimama na kumshangilia kwa makofi na nderemo.
Chambilecho Marehemu Ken Walibora (Mungu ailaze roho yake pema),siku nyingine njema ilikuwa imemfikia Hafsa.
Baada ya hapo, wote waliandamana unyounyo hadi kwenye karamu iliyokuwa imeandaliwa kwa heshima ya wanakereketwa wote kwa jumla.
Walikula,wakanywa,wakazungumza na pia kunengua viuno.
Jina Hafsa likawa limeandikwa kwenye kumbukumba za historia ya kimataifa.

************************************
Haukupita muda mrefu baada ya Hafsa kutunukiwa, kabla ya kuteuliwa na Umoja wa Mataifa kama balozi wa haki za watoto.
Majukumu yake yakiwa kuangazia maswala ya haki za watoto kote duniani.
Akawa kiguu na njia kuhudhuria vikao na mikutano mbalimbali kote duniani.
Hafsa akawa sauti ya Umoja wa Mataifa, hasa kuhusu tamaduni zilizowakandamiza watoto,ajira kwa watoto na kutumiwa kwa watoto kupigana na waasi wa kivita.
Kipindi chake kikapata watazamaji na washiriki kutoka pembe zote duniani.
Kutokana na majukumu haya mapya,Hafsa alijiuzuru kutoka kituo cha habari alikokuwa akifanyia kazi na kuhamisha kipindi chake hadi mtandao wa 'YouTube'.
Hili lilimwezesha kuvirekodi vipindi vyake kutoka eneo lolote duniani.
Pia lilimwezesha kufikia watazamaji kutoko mataifa yote,bora tu,wawe na mitandao ya intaneti.
Marie alikuwa tayari kapata riziki kama mpondozi wake Hafsa na wageni katika kipindi chake.
Mavazi yaliyotengenezewa katika kampuni yake,yakawa yanampamba Hafsa, Suzzanna na Bundi.
Kupitia kwa Jason,Maria aliweza kuanzisha duka la mavazi kule Marekani.
Mavazi haya yalikuwa na dhima za kiafrika.
Mchanganyiko wa Kiafrika na mitindo ya kisasa ya kimavazi.
Kwa jinsi yalivyomvaa Hafsa,Marie alipata wateja watazamaji wa kipindi cha Hafsa,watimtaka kuwatengenezea mavazi kama yale.
Marie akatambaa na kuwa jumba la mavazi tajika duniani.
Mitindo yake ya mavazi akawa anaiita 'Afrodunia designs'.
Asiye macho aliambiwa atazame kwa kuwa mitindo hii ilienea kama moto nyikani,hasa kwa wasanii Waafrika.

************************************
Hafsa aliwahi kuwahoji Suzzanna na Bundi kwa mara nyingine katika kipindi chake.
Mahojiano yaliyowapatia umaarufu wa kuweza kupata ufadhili wa kifedha na kimawazo,kutoka mashirika ya kimataifa.
Walilenga kujenga hospitali ya kushughulikia afya ya kiakili,pamoja na kuanzisha chuo cha kufunzia wataalam wa saikolojia na afya ya kiakili.
Hafsa akawa daraja ambalo kwalo,milango ya fanaka iliwafungukia wenzake.

Wakati huu Suzzanna na Bundi walikuwa wameyakamilisha masomo yao na kujiingiza kikamilifu katika shirika lao.
Uhusiano wao pia ukawa umekomaa na kuanika maua.
Kwa kuwa kwa sasa, hawakuwa watoto tena, gumzo kuhusu kufunga ndoa likawa linawaandama vinywani mithili ya vivuli vyao.
Urafiki wao ulikuwa umepitia kiangazi na masika; hivyo, ilitarajiwa kuwa ndoa yao ingefaulu.
Tayari walikuwa wameshiriki katika sherehe zote za kuposiana na wakapata baraka kutoka kwa wazazi wa pande zote mbili.
Kipindi hiki kilikuwa cha umuhimu mkubwa kwa Suzzanna kwani alikuwa ametimiza ahadi yake ya ubikra kwa Bundi.
Bundi licha ya kutegwa na ibilisi katika miaka yake ya mwanzo chuoni,pia aliweza kutimiza ahadi yake ya ubikra wa pili.
Wakati mwingine ubikra ni maamuzi ya kuacha kufanya tendo na wala si katika kiungo cha mwili.
Kuna ubikra wa kimawazo ambao uletwa na kujaza fikra kwa mawazo mema na ya matumaini.
Ubikra huu ni muhimu sana katika kudumiza utimamu wa kiakili.
Kuvunjwa kwa ubikra huu,ndio huleta tatizo la kusongwa na mawazo akilini.
Ni ubikra ambao Bundi na Suzzanna walikuwa wamejitolea kuwarejeshea waathiriwa.
Mipango ya harusi ilikuwa imekamilika, kwa marafiki hawa wawili,wa tangu utotoni.
Waliingojea siku yenyewe kama angojeavyo,kitoto chake kutambaa baada ya kuzaliwa,kwa mama mzazi.
Je kitoto cha penzi lao hatimaye kingetambaa,kuchechemea na kisha kutembea wima?

SUZANNAWhere stories live. Discover now