Sura ya Kumi na Tatu

18 1 0
                                    

Mji wa Melbourne ndio mji wa pili kwa ukuu nchini Australia.
Humu ndimo Chris alipata makao yake mapya huku akifanya kazi katika hospitali moja ya kibinafsi kama daktari msaidizi.
Mazingira ya kazi na maisha katika mji huu yalikuwa ya kuvutia mno.
Miundo msingi ilipangwa ikapangika na kila shughuli iliendeshwa na kusimamiwa kwa ustaarabu wa hali ya juu.
Makazi viungani mwa mji yalitawaliwa na miti na maua yenye rangi mbali mbali.
Ilikua ni Kama kuishi bustanini.
Siri na uchafu  wa mtungi aijuaye ni kata.
Chris alikuwa na siri moja ambayo, aliyeijua ni katake Rosata na Suzzanna.
Hakuwa ametua  Melbourne kujipatia riziki tu!
Alikuwa na tatizo sugu ambalo alitamani kulitegua kuku huku.
Mashine yake  ilikua haingurumi wala kufua dafu hata kama vibaya vibaya.
Alijiona na kujihisi mwanaume nusu.
Ni tatizo lililompa kiunzi hasichoweza kukiruka katika mbio za mapenzi.
Alienda Australia kuchapa kazi na pia kusaka tiba.
Alitamani kupata tiba ambayo ingemwondolea haya na fedhea usoni, ili kuwa jogoo la kuwika saa kenda usubuhi na kusikika kama jogoo wengine.
Kila jogoo huwika ili kutambulisha uwepo wake na kuwaonya jogoo wenzake kutowakaribia koo wake.
Kila mwanaume ni jogoo kwake eti!

Swali ni je,jogoo huwa jogoo kwa sababu ya uwezo wa kuwika,au kwa sababu aliumbwa akiwa jogoo?

Chris alibahatika kuwa na rafiki wa dhati ambaye alihifadhi siri yake, hasimwambie mtu mwingine.
Rosata alikuwa kata la dhahabu kwake,na  msiri wake mkuu.
Kwa kuwa Chris alikuwa na ulemavu wa kifaa cha kuchezea ngoma ya mapenzi,wawili wale walitafuta mbinu mubadala ili kuzikimu haja zao za kimapenzi.
Kuvunjika kwa mwiko sio mwisho wa kusonga sima eti?
Sima ya mapenzi waliweza kuisonga,na pengine kwa ufundi wa kushibisha matumbo yao ya usuhuba kuliko waliotumia mbinu za kawaida.

Sima inapoandaliwa, kufuata utaratibu uliopendekezwa kwenye recipe ndilo jambo la umuhimu wala si matumizi ya mwiko.
Kwanza lazima kuchemsha maji hadi kutokota.
Sima iliyotengenezwa kwa maji baridi huwa haina ladha.
Huoneka kama gamu gamu.
Pili,kiwango cha unga wa mahindi kinachofaa lazima kutiliwa kutegemea kiwango cha maji.
Ni muhimu kuhakikisha kuwa maji hayazidi unga au unga kuzidi maji.
Tatu,kwa kutumia mwiko au kifaa kingine,ukorogwa hadi kushikamana.
Kuna wale hukoroga kwa kasi na wengine hukoroga kwa mwendo wa aste aste,bora tu,unga kulowa na kushikamana barabara.
Nne,sima hupinduliwapinduliwa kwa zamu hadi kutokota na kisha kuachwa kuiva hadi kuzua mvuke wa kunukia.
Hapo sima huwa tayari kuandaliwa.
Chris alikuwa hapa Melbourne ili kurekebishiwa mwiko wake kuweza kuisonga sima kama wasongaji wengine,kwa mbinu ya kawaida.

***********************************
"Ni mboni zangu zanicheza vifumba macho,ama kweli yule ni Mathangi?" Chris alijiuliza huku akiitoa miwani yake kuipanguza kuona vizuri.

Chris alikuwa katika pitapita zake alipomwona mtu aliyefanana  Mathangi,akiingia katika treni aliyokuwa akiabiria.
"Kama kweli ni Mathangi,anafanya nini huku Australia?" alizidi kujikuna akilini kukitegua kiini macho kilichokuwa mbele yake.
"Nadhani nitamkaribia ili niweze kumwona vizuri na pia kufahamu fika atakakoshukia" Chris alianza mwendo wa kumkaribia Mathangi ili kumpiga darubini la Karibu.
Kwa kuwa gari moshi likikuwa limejaa, Mathangi alisimama kwa kujisitiria kwenye vishikio vilivyotundikwa sehemu za kusimama.
Chris alimkaribia na kumtazama kwa karibu.
Alimwona ni Mathangi si Mathangi.
Kidogo, alikuwa mrefu kuliko Mathangi,na mweupe zaidi kuliko Mathangi.
Macho yao yalikutana, ila Mathangi hakuonyesha dalili zozote za kumtambua Chris.
Mathangi alikuwa amevalia kitambulisho shingoni kilichoandikwa,Dr.C.Mathangi.
Shaka lilizidi kumvaa Chris,kwa kuwa Mathangi aliyukuwa mwalimu wake alikuwa Dr.J.Mathangi.
Mtihani wa kumtambua Mathangi ukazidi kuwa mgumu.
Wote wawili walishukia kwenye kituo kimoja na kufululiza hadi kwenye hospitali ambapo Chris alikuwa afanyiwe upasuaji.
"Ahaa kumbe jamaa ni daktari hapa!Nitaweza kumfichua hata kwa urahisi kuliko nilivyokuwa nikitarajia" Chris alijipa moyo.
Chris alikuwa hapa kufanyiwa uchunguzi wa hali yake ya afya kama matayarisho ya upasuaji ambao ungefanyika katika wiki mbili zilizofuatia.
"Everything seems ok Doc Chris" muuguzi alimpatia matokeo ya uchunguzi huku akimpapata mabegani.
"You said you from Kienia, right?" muuguzi aliendelea.
"Yes I am" Chris alijibu huku akinyoosha mikono ya shati lake iliyokuwa imekunjwa.
"Am asking because the lead surgeon in your operation is Dr.Charles from Kenya" muuguzi alielezea.
"Would you like to meet him today?He just checked into his office" muuguzi aliendelea huku akifungua mlango kumwelekeza Chris kakita ofisi ya Dr.Charles.
Dr.C.Mathangi.
Maandishi yaliyokolezwa yalimkondolea Chris macho,langoni mwa ofisi kabla kuingia.

"Vipi ndugu?Karibu sana,Mimi ni Dr.Charles kutoka kwenu bana!" Mathangi alimkaribisha Chris.

Baada ya mazungumzo ya muda,Chris aliweza kung'amua kuwa Dr.Charles alikuwa ndugu pacha,wa toka ni toke wa Dr.James Mathangi,mkimbizi wa uhuni.
Charles hakuwa na habari yeyote kumhusu James licha yakuwa walikuwa wakiwasiliana mara kwa mara.
Ilikuwa afueni kwa Chris.

************************************
Rosata alisafiri kuelekea Australia ili kumuuguza rafikiye Chris.
Licha ya kujikakamua na kushamiri katika uchezaji densi,malengo yake yaliotea vibaya.
Jason alikuwa amezamia kwenye mapenzi ya Maria asiweze kusikia la Rosata wala la bibiye aliyemwacha Marekani.
Jason aliyapenda maisha ya kuangaziwa na kuvutia vyombo vya habari.
Sekta ya utumbuizaji ilikuwa imemkubali na kumpiga pambaja, hasa baada ya Maria kusemekana kuwa na ujauzito.
Majarida na mitandao ya Ulimbwende yaliangazia maisha yao, kama watabiri wa hali ya anga waangaziavyo mabadiliko katika mikondo ya mawingu angani.
Kila walipoonekana,hata kama wakitoka msalani, paparazzi waliwaandama angalau kupata picha ya kipekee.
Yote haya yalimchosha Rosata,akajihisi kama aliyejaribu kulingoja jabali kuyeyuka ili kupata maji.
Ujio wake kwa Chris ukawa mwanya wa kumzika Jason katika kaburi la sahau ili kuanza maisha mapya.
Alitarajia Chris angepona na kisha waishi kama mke na mume.
Gangaganga ya Rosata ilimwacha Chris kwa matumaini ya kutaka kupona hata kwa upesi zaidi.
Daktari Charles alikuwa amemwakikishia Chris kuwa tatizo lake lingeisha, kwa kuwa lilikuwa dogo tu!
Mshipa wa damu haukuweza kufikisha damu ilivyostahili ili kusisimua ume wake.
Rosata alikuwa bako kwa bako akingoja siku ya afueni ya Chris.
Alitaka awe wa kwanza kukiabiria chombo cha uroda cha Chris.
Uvumilivu wake ulifua dafu kwani baada ya takiban miezi miwili, chombo cha Chris kilinguruma na kupaa  bila wasiwasi wala kasheshe.

Rosata na Chris walianza musakato wao wa kuisonga sima kwa utaratibu.
Ilikuwa mara yao ya kwanza kabisa kuisonga sima kwa kutumia mwiko.
Shughuli ambayo waliifanya kwa uangalifu mkubwa,ili wasije wakaiunguza sima.
Ilikuwa furaha iliyoje kwa wawili wale kuketi sebuleni, kufurahia kopo la maji ya matunda na mvinyo,baada ya shughuli nzima?
Walichoka wakachokeana,na kubaki kubugia vinywaji vyao,huku Rosata kajikunyata,kichwa kakiekelea juu ya kiwiliwili cha Chris.
Mkono wa kulia wa Chris ulinyanyua glasi hadi mdomoni na kisha kuirudisha mezani, huku ule wa kushoto ukipapasapasa nywele za kifarasi zilizomjaa Rosata kichwani.
Kwa sasa nywele zenyewe zilichakaa na kuenekana kama matuta meusi yaliyopendeza.
Rosata hakuwa na haja ya umaridadi wa nywele kwani alikuwa amepeperuka na kutua katika dunia ya raha msaterehe.
Baada ya kupumzika, Chris na Rosata waliamua kuisonga sima kwa mara ya pili,pale pale kochini.
Chovyachovya ya asali haikomi hadi kulimaliza buyu.

************************************
Fungate ya Bundi na Suzzanna ilikuwa ya kufana mno kule visiwani Ngazija.
Kwa miezi miwili waliweza kujitenga kutoka kwa ulimwengu wa watu wengine na kuzamia katika ulimwengu wao.
Walimwachia mkurugenzi,shirika lao,kuliendesha chini ya uangalizi pevu wa Mgema.
Walikuwa wamengojea ndoa yao kwa miongo mingi,hivyo walikuwa na kila haki ya kupata wakati mwanana kufurahikiana.
Ngoja ngoja yao haikuwaumizia matumbo hata kidogo.
Uhusiano wao ulikuwa kama mvinyo uliochocha baada ya kuhifadhiwa bewani kwa muda mrefu.

Hafsa aliandamana nao, ili kunasa starehe yao na kupepurushia mashabiki wake moja kwa moja.
Hafsa, hakuwa ameyapanga haya,bali alisukumwa na watazamaji wake,hasa baada ya kuwapeperushia harusi ya kipekee pale awali.
Utazamaji wa kipindi chake ulikuwa umekua mara dufu.

Mmoja wa mashabiki ambao hawakukosa kukitazama kipindi,ni Jason.
Kila alipomtazama Suzzanna wakiwa na bwanake,alikimeza kifundo cha mate na kutamani kuwa angekuwa  yeye katika nafasi ya Bundi.
Mapenzi ya utotoni yalimkwama kama ndwele lilisiloskia dawa.
Dawa yake ikawa haipatikani tena kwani tayari ilikuwa imemilikiwa na Bundi kujitibia maradhi ya roho yake.
Umakinifu huu wa Jason kuhusu fungate ya Suzzanna, ulimtia kiwewe Maria na kuleta mafarakano ya mara kwa mara kati yao.
Mara nyingi Maria alijisingizia kuumwa ili kuvutia makini ya Jason.
Uhasama uliokuwa kati ya Maria na Suzzanna juu Jason nyakati za shule, ulionekana kutibuka usaha kwa mara nyingine.
"Jas, Suzzanna sasa ni bibi ya wenyewe,uko na mimi,the sooner you accept that the better" Maria alimwita Jason kwa jina la utani na kununa.
"Am just benchmarking babe,yetu itakuwa ya kukata na soka.Itakuwa katika Dubai ama Bahamas,si Afrika" Jason alimuliwaza Maria na kumwachia tabasamu rohoni.

SUZANNAWhere stories live. Discover now