SUZANNA

By MhengaRukaria

546 23 0

Suzzanna ni kielelezo cha mtoto msichana wa kiafrika na changamoto anazokumbana nazo maishani. Ni tumaini kuw... More

Sura ya kwanza
Sura ya Pili
Sura ya Tatu
Sura ya Nne
Sura ya Sita
Sura ya Saba
Sura ya Nane
Sura ya Tisa
Sura ya Kumi
Sura ya Kumi na Moja
Sura ya Kumi na Mbili
Sura ya Kumi na Tatu
Sura ya Kumi na Nne
Sura ya Kumi na Tano
Sura ya Kumi na Sita
Sura ya Kumi na Saba
Suzzanna Sura ya Kumi na Nane
Sura ya Kumi na Tisa

Sura ya Tano

22 2 0
By MhengaRukaria

Siku ya upasuaji wa Suzzanna kama ilivyoratibiwa na daktari  Mathangi iliwadia.
Mathangi alihakikisha kila alichokihitaji kufanya upusuaji kilikuwa tayari.
Kitanda cha kumlaza mgonjwa kilikuwa kimetandikwa na hata kupuliziwa manukato yaliyoacha mapua wazi kwa mvutio.
Koja la maua lilijipanda pembeni,likiashiria ni chumba chenye uhai na starehe.
Godoro aina ya 'Dreamland' lilikilalia kitanda na kukifanya kunyooka twa! tayari kumkandakanda  mgonjwa na kumwacha katika usingizi wa pono.
Shuka za rangi nyekundu zilikivaa kitanda na kukifanya  kuonekana kama tandiko la malkia kwenye kasri.
Mziki aina ya 'blues' uliyoimba na sauti za kumvutia nyoka kutoka pangoni,uliporomoka kutoka kwa radio aina ya 'Sonnymax'.
Mvinyo aina ya 'red wine' ulikuwa umeandaliwa kwa unadhifu,ukiambata na glasi mbili tayari kumutumbuiza mgonjwa na kumuliwaza ili kumfanya kupitia upasuaji bila haya.
Mataa yaliyomulika kwa mwanga mwekudu na samawaki yalimetameta kwa zamu na kukipaka chumba cha upasuaji kubadilibadili rangi kama kinyonga.
Kila kitu chumbani kikichukua rangi za mataa kisitambulike rangi yake halisi.
Kinyume na mazoea katika upasuaji wa hapo mbeleni;wakati huu Mathangi hakukusudia kuvalia glavi katika mikono yake.
Angefanya upusuaji mikono uchi.
Pengine alimwamini mgonjwa huyu zaidi,kuamini hangemwambukiza maradhi yeyote.

"Kokoko"  mlango ulibishwa kwa mpigo dhaifu.
Mgonjwa alikuwa keshawasili.
Mathangi alikipiga macho chumba chote kuakikisha kila kitu kilikuwa sawia,kwa mara ya mwisho,kisha akaelekea mlangoni kumkaribisha mgonjwa.
Kulikuwako na kamera ya siri mlangoni iliyomwezesha kutimazama aliyekikaribia chumba hiki akiwa mbali.
"Karibu,Karibu ndani Suzzie" alimpiga pambaja haraka haraka huku akimunyooshea mkono kumkaribisha ndani.
Alichunguliachungulia nje kwa mpepesuko, kuhakikisha kuwa hakukuwa na mtu mwingine karibu, kabla ya kuufunga mlango kwa funguo.
"Wao this place looks so romantic" mgonjwa alitamka huku akizungukazunguka chumbani,akichezachezesha kiuno kuandamana  mdundo wa mziki uliokuwa ukiporomoshwa kwa sauti nyororo ya Lionel Richie.
"Karibu kwa kitanda" Mathangi alimkaribisha huku akimkabidhi glasi iliyojazwa mvinyo.
"Ahsante!" mgonjwa aliketi pembeni mwa kitanda na kuuweka mguu mmoja juu ya mwingine na kuyawacha mapaja yake meupe pepe!wazi.
Msisimko ulimpanda Mathangi na kumwongezea matumaini ya kukamilisha upasuaji huo.
"You look so lovely!" Mathangi alitamka huku akiupitisha mkono wake juu ya mapaja ya mgonjwa.
Mgonjwa hakumzuia bali alimwacha kujibamba.
Mgonjwa alipiga funda kubwa la mvinyo huku akisimama na kumkalia daktari mapajani.
Unyororo na joto la makalio lilimwacha daktari akidodokwa na mate.
Ili lilimpata Mathangi kwa mshangao.
Mambo yalikuwa yanaenda upesi kuliko alivyotarajia.
Akiupitisha mikono wake katika kiuno cha mgonjwa na kuyakamata maziwa yake huku akiyafinyafinya kwa utaratibu.
Mgonjwa aliachilia sauti ya kuridhika na kupumua huku akifunga macho.
Uhodari wa mokono ya daktari ulimfanya kuisahau ghadhabu yake kwa muda.
Mikono ya daktari ilipofikia nywele zake za kifarasi, mgonjwa alisimama haraka kujinasua.
Palikuwepo kamera ya kisiri katika nywele zake iliyotumiwa na majasusi kufuatilia sinema hii.
"Naomba twende kwa upasuaji moja kwa moja kwa sababu nina shughuli zingine" mgonjwa aliomba huku akimrusha daktari kifudifudi kitandani.
Alilifungua shati la daktari huku akimpapasapapasa kwa vidole vyake vyororo.
Kwa zamu walivuana nguo na kubaki uchi wa nyani tayari kuuanza upasuaji.

"Taptap!taptap!" sauti za watu wakikaribia kwa utaratibu zilisikika.
Mathangi alimrusha Suzzie pembeni na kukimbilia mlangoni kuchungulia akitumia kamera ya siri.
Aliwaona wanaume watatu na wanawake wawili waliojihami kwa bastola wakikaribia mlango.
Nyuma yao wanahabari walifuata unyounyo tayari kunasa uvamizi huo.

Suzzie aliangukia meza na kuumia vibaya.
Kamera iliyobandikwa nyweleni ilivunjika na kutapakaa vipande vipande,juu ya michirizi ya damu iliyomtoka Suzzie kichwani.
"Pu!" makachero waliupiga mlango dafrau na kujitosa ndani wazimawazima tayari kumkamata Mathangi.
Mathangi hakuwepo.
Walitaftatafta chumba kizima wasimpate.
Suzzie alikimbizwa hospitalini akiwa amepoteza fahamu.
Baada ya uchunguzi wa kina majasusi waligundua mpenyo wa chinichini kule chumbani,alioutumia mshukiwa kukwepea.
Mathangi alikuwa amewaponyoka.

**********************************
Habari hizo zilienea kama moshi jangwani, katika mitandao ya kijamii na vyombo vya habari.
'Muhadhiri mkware awahepa makachero baada ya kufumaniwa na mwanafunzi' vilisoma vichwa vya habari.
Baada ya kisa hiki,mamia ya wanafunzi walijitokeza kupasua mbarika kuhusu masaibu yao kutokana na 'alama za ngono'.
Ilitambulika kuwa ni saratani iliyokuwa imetawala katika vyuo vingi,hasa Afrika.
Chini ya heshitegi #SexGrades; waathiriwa wengi walijitokeza na kueleza waliokumbana nayo katika vyuo vyao.
Visa vingi vya kutamausha vilijitokeza na wahadhiri wahusika kutajwa bayana.

Mmoja wapo wa waathiriwa alikuwa ni Charita, ambaye kwa sasa alikuwa Mwanauchumi mtajika.
Alielezea kwa uchungu mkubwa jinsi Abedi, Mchungaji mla kondoo,alivyomfanyia unyama, alipoenda kutafta ushauri kwake.
Charita alikuwa yatima aliyewapoteza wazazi wake kakita mapigano ya kikabila baada ya uchaguzi.
Familia yake ilikuwa moja ya  madodoa yaliyolengwa kuondolewa kulingana na wachochezi wanasiasa.

Babake alikuwa mfanyabiashara aliyenunua shamba katika eneo tofauti na alikozaliwa na kujenga jumba la kifahari.
Walikuwa wanajiweza kimaisha na kuishi maisha ya hali ya juu.
Wakati wa siasa majirani waligeuka na kuwa mahasidi waliowangamiza.
Kisa cha asubuhi hio ya mwaka wa elfu mbili na nane kilimsumbua na kumukoseza usingizi Charita.
Yaliotukia yalijirudiarudia akilini mwake kila alipolala au kutulia.
Alishuhudia kila kitu asijue la kufanya.
Asubuhi hiyo,genge la wenyeji,wakiwemo majirani,walivamia maakazi yao na kuteketeza kila kitu,walikiwemo wamiliki.
Wazazi na ndugu zake waliteketezea kiasi cha kubakia jivu.
Charita aliponea kwa kuwa wakati huo alikuwa amekwenda shambani kutafta matunda.
Duru walizozipiga  zilimkwama kama doda sugu akilini.
Aliokolewa na msamaria mwema aliyemfikisha kwenye makao makuu ya Askofu wa Kikatoliki, walipopewa hifadhi waathiriwa wengi wa mchafuko huo.
Charita alikuwa amemwendea Abedi akimtaka kumwombea na kumshauri kuhusu tatizo la kiakili, lililomwadama asiweze kumakinika masomoni.
Badala yake, Abedi alichukua fursa hiyo na kumnajisi huku akimwonya kuwa,angetoboa unyama huo,basi Abedi angekatiza msaada wake wa masomo uliokuwa ukitolewa kupitia afisi yake.
Charita akawa hana budi ila kutia zii,hadi wakati huu ambapo aliupata mwanya wa kumkabili ibilisi, Mchungaji mla kondoo.
Kidagaa cha Abedi kilikuwa kimemwozea,kwani alipigwa kalamu na kufunguliwa mashtaka.
Kwake Charita,siku njema ilikuwa umefika.
*********************************
Mathangi alifaulu kukwepa mtego wa makachero na kuchania mbuga nchi jirani akitumia 'bodaboda'.

Kwanza, alitorokea mji wa mpakani ambapo alijificha kwa muda kabla ya kuvuka boda kwenda mafichoni.
Nyuma aliwaacha mke na watoto wawili, ambao maisha  yaligeuka kutoka na ukiritimba wa jamii.
Kila walipopita,waliowafahamu waliwasengenya na kuwaangalia kwa kinyaa.
Marafiki waliwakwepa,wakabaki wametengwa kama wagonjwa wa kifafa
Maisha yakawa magumu kwa wanawe katika shule walikosomea.
Wakachekwa na wenzao na kubandikwa majina ya kejeli.
Ilimbidi mama yao kuwatoa shuleni kwa muda,ili kuwataftia shule nyingine.
Maskini wakaubeba msalaba wa dhambi za baba yao.

Kule Uganda, Mathangi alijihusisha na biashara ya kuuza nyama  kijijini alikopewa hifadhi na rafiki yake wa zamani.
Alibadilisha hulka yake kutoka udaktari,ila alilivaa lilelile kabuti jeupe kuuzia nyama.
Alibadilisha jina lake na wenyeji wakawa wanamwita 'daktari',bila kufahamu alikuwa daktari wa ukweli.
Biashara yake ilinawiri mno.
Alinuia kufanya biashara na kukusanya pesa ambazo angezitumia kutorokea ughaibuni,kurejelea kazi yake ya uhadhiri.

***********************************
Suzzanna alisalia hospitalini kwa muda wa miezi miwili.
Kuanguka alikoanguka kulimwacha na jeraha kichwani.
Jeraha ambalo lilimlaza katika chumba cha wagonjwa mahututi kwa mwezi mmoja.
Alikuwa hajijui wala kujitambua.
Alifanyiwa upasuaji, ambao kwa wakati huu,ulikuwa wa kuondoa damu iliyoganda ubongoni.
Upasuaji ulifaulu na alitarajiwa kupona kabisa.
Wendani wake,Bundi na Chris walisimama naye kidete, wakimtembelea kila wakati.
Ikawa ni zamu ya Bundi kumjali na kumushughulikia rafiki yake.

Rosata alitukia kuwa kiegemezi  cha kutegemewa wakati huo.
Rosata alikuwa na kipawa cha utunzi na uimbaji.
Kila mara akitunga na kumwimbia Suzzanna nyimbo na mashairi ya kumtia moyo na kumuliwaza,akiwa katika sitofahamu kule 'ICU'

"Suzzanna kipenzi,kiumbe uliyeumbika
Kakuumba jalali na urembo kukutunuku.
Kipawa kakubidhi,nayo mengi maarifa.
Ni majukumu maridhawa,alokundea kuyakamilisha.
Nakuembea siha halili,urudi kuendelea
Dunia yakungojea,wema wako kupambia."

Jason alijitolea kugharamia matibabu yote na pia kuhaidi matibabu zaidi kule Marekani.
Kwa Sasa Jason alikuwa mmoja wa wachezaji wakwasi zaidi wa kiafrika kule Marekani.
Alikuwa ameanzisha 'Jason Foundation',kwa madhumuni ya kukuza na kutambua talanta katika watoto Afrika, pamoja na kuwasaidia kupata nafasi za kung'aa Uropa na Marekani.

Hafsa angetoa huduma zake za uwakili kuhakikisha haki ingepatikana kwake Suzzanna na waathiriwa wengine.
Je mkono mrefu wa Sheria ungefaulu  kumchimbua Mathangi alokojificha?

Masaibu yaliyowakabili mkewe Mathangi na malaika wao wawili,yalitoa nafasi kwa Bundi na wenzake, kuwasaidia kupitia kwenye lindi la fedhea walioletewa.

Ama kweli akufaaye kwa dhiki ndio rafiki.

Continue Reading

You'll Also Like

141 1 6
Msururu wa hadithi unaozungumzia kudorora kwa haki,ukosefu wa matumaini,dhuluma pamoja na utapeli unaoendeshwa na viongozi dhidi ya wananchi. Kauli M...
113 2 16
Maya ni daktari aliejikuta katikati ya marafiki wenye wazazi mahasimu.Maisha yake na misimamo yake vilimlazimu kuwa na hikima upole ukatili usiri na...
18 0 3
Hadithi ya ubunifu kungazia maswala na changamoto zinazoukaili ulimwengu katika karne hiii
546 23 19
Suzzanna ni kielelezo cha mtoto msichana wa kiafrika na changamoto anazokumbana nazo maishani. Ni tumaini kuwa licha ya changamoto hizi pana njia iwe...