Translation Games: Kiswahili

9 5 0
                                    

Big Bang by BrianMullin0

Language: Kiswahili

Translated by: Lujayna


Mlipuko Mkuu

Iliyotafsiriwa na: Lujayna

Gargul, kijana aliyekuwa mungu wa anga-nje aliangalia alichofanya na kukuna kalio lake. Chakuvutia ni kuwa alichotenda kilikuwa bado kina utegili pembeni. Sayari trilioni sita, zote zikizunguka nyota kubwa iliyokaa kama imeoza. Takribani bilioni za sayari zina uhai. Kama uhai huo utadumu na kuendelea, hakujali.

Ukweli ni kuwa, hakutia bidii. Hakuyafikiria wala kuyapanga. Snood alikawiya kwa muda mrefu akiyapanga, na B'larbarra alitumia wakati mwingi zaidi kuchagua rangi. Yeye alihisi tumbo likivimba na akafanya haraka!

Milipuko Mkuu mwipya.

Viumbe vingine ni kama maua yakunukia vizuri.

Na malimwengu mengine yatisha.

Tevun-Krus #108 - International 7: The Big Bang!Where stories live. Discover now