STORY: *MALIPO*
MWANDISHI: *IRENE SYILIVESTER MBUYA*
*SEHEMU YA 01*
Nilizaliwa katika familia ya wazazi wenye uwezo kwa waliokuwa wakinifahamu walijua natokea katika familia moja ya kitajiri sana,katika maisha yangu ya utoto nilikua na sifa moja mbaya ya kunyanyapaa watoto waliotoka katika familia zenye shida. Sikutaka kujumuika nao katika chochote tabia hii haikuwa mtaani tuu bali hata shuleni nilikua vivyohivyo. Baadhi ya walimu hawakunipenda ila hawakuwa na cha kunifanya nilijivunia Baba yangu ambae alikuwa kiongozi serekalini na Mama yangu alikua miongoni mwa madaktari bingwa. Niliendelea ivyo hata kumaliza elimu ya awali na kuingia ngazi ya sekondari. Kwa kipindi kile nilikuwa na mitazamo mingi sana nilijua kuna siku nitakuwa bosi,nitakuwa na miradi yangu mbalimbali,nitakuwa na jumba kubwa la kifahari na magari mengi tuu,sikuwahi kufikiria kuna siku nitakuwa omba omba. Maisha haya basi tuu kwani utafikiri upepo ulipita mkali na kubadilisha kila kitu,maisha yalibadilika ghafla mara baada ya wazazi wangu wote wawili kufariki baada ya kupata ajali mbaya sana ya gari baada ya gari kuacha njia na kuingia korongoni ili hali kulikuwako na mvua kubwa sana. Hapo nilikua kidato cha pili mara ghafla niligeuka chokoraa kwani sikuwa na mtu wa kuniendeleza kimasomo mali zote zilibinafsishwa na mashirika mbali mbali ikidaiwa kuwa wazazi wangu walikuwa wakidaiwa pesa nyingi sana. Sikuwa mtoto pekee ila nilikuwa na wadogo zangu wawili Julian na Mike. Julian kwa sasa ni marehemu na Mike mpaka dakika hii sijui ni wapi aliko. Ndugu walitutenga sikuwa na mtu wa kumgeukia kulingana na nilivyokuwa na tabia za ajabu enzi za uhai wa wazazi wangu. Nilianza kurandaranda kwetu kiporo kilimwagwa lakini ilifika mahali nilikula dampo na wakati mwingne ni chakula kilicho chacha tayari. Hakuna siku ambayo sikulia katika kumbukumbu zangu nilikutana na wakati mgumu sijawahi ona kwakweli. Na nilikutana na mambo mengi ambayo kwa umri ule wa miaka 16 yalikua ni changamoto kubwa sana kwangu. Usiku mmoja nilikutana na dhahama moja ambayo ilinifanya nitamani kufa lakini sikufa ila ni kitu siwezi sahau maishani mwangu. Nilikutana na wahuni walichonifanyia kimebaki kama kovu ndani ya moyo wangu. Tangu siku hiyo sikuwa na amani tena nilijitenga na kukaa mbali na watoto wengine wa mtaani katika pita pita zangu nilikuta nyumba moja mwenye nyumba ile nilimtambua alikuwa akifahamiana sana na marehemu mama yangu. Nilienda kumsalimia
"Mama shikamoo"
Aliniangalia kwa dharau juu mpaka chini ila hayo sikujali mimi nilitaka tuu anisaidie kitu kimoja nilirudia kumuamkia
"Shkamoo mama"
"Namfanania mama yako mimi?"aliniuliza kwa ukali
"Nisamehe kama nimekosea ila nilikua na shida moja mama tafadhali nisaidie"
"Hahahahaha eti shida moja hivi wewe alikuambia nani hapa natoa misaada?"
Kwa bahati nzuri mume wake alitokea na kwa wakati huo nilikua naondoka kwani nilichowaza sicho,mume wake aliniita
"Getrude!!"
"Bee Baba" niligeuka kumtizama
"Una shida gani mwanangu?" Aliniuliza kwa upole tuu ila mkewe alidakia
"Mwanao kwa tumbo la nani?"
"Hivi unaroho gani we mwanamke huyu mtoto humjui? Wakati unakula maisha na wazazi wake ulimuona mtoto si ndio?" Mume wake alimuuliza
"Huyu mtoto? kokoto? Hahahah ya leo kali sasa msaidie utakachomsaidia ila hiki kijini ndani kwangu staki kukiona" yule mama alisonya na kuondoka kwa ghadhabu.
Kwa maneno yake yalivyokuwa makali huku nikikumbuka ambavyo alikuwa akija kumlilia shida mama yangu na mama yangu alimsaidia wakati mwingne familia yake ikiuguwa mama aliwatibia bure ila kasahau yote,nilijisemea moyoni *'kwanini wazazi wangu mmeniacha niteseke peke yangu'* yule baba alinibembeleza sana kila aliposema nyamaza ndipo moyo ulipozidi kuumia. Aliniuliza nilikuwa na shida gani nilimwambia
"Julian ni mdogo sana baba naogopa kuwa kuna siku atapata tatizo kubwa sana naomba nisaidie kumlea mimi na Mike tutapata tuu sehemu tuishi na hata huku mtaani sisi tunaweza vumilia ila kwa Julian ni ngumu mbaya zaid sio kila mda tutakaa nae muda mwingine tunatoka kwenda kuomba vyakula kwenye migahawa ili tumletee ale kwani yeye hawezi kwenda kutafuta kama sisi"
"Kwani yuko wapi?"
"Nilimuacha ndani ya pipa kule dampo"
"Ndani ya pipa dampo?!"
"Ndio baba"
"Nenda kamlete utanikuta hapa hapa nje ya geti"
Nilikimbia kama sina akili nisingeweza kumlea Julian katika maisha yale ukizingatia nilishaogopa kutokana na nilichofanyiwa nilienda na kumchukua Julian na kwenda nae adi kwa baba yule nilimkuta nje ya nyumba yake kama alivyoniambia
"Sasa Getrude mdogo wako yuko mikono salama uwe na amani kabisa"
"Asante sana baba Mungu akubariki sana"
Niliondoka huku nikilia sikutegemea kama kuna siku familia yangu ingesambaratika kama majani makavu yapeperushwavo na upepo.
*Usikose sehemu ya 02 ya Malipo ili kujua nini kitaendelea*
BINABASA MO ANG
MALIPO
Mystery / ThrillerGetrude ni msichana aliyepitia wakati mgumu sana kwenye maisha yake ikiwa kama malipo ya jinsi alivyokuwa na roho ya kishetani kipindi wazazi wake walivyokuwa hai
